MADIWANI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUCHOSA WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA YA MAADILI

Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya ZiwaBwana Godson Kweka amewataka Madiwani na watumishi wa Halmashaui ya Buchosa mkoani Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika utekelezaji wa Majukumu yao.
Bwana Kweka ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa mafunzo juu ya uzingatiaji wa maadili kwa Waheshimiwa Madiwani na watendaji wengine wa Halmashauri hiyo.
Aidha Bwana Kweka alifafanua kuwa, Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa kuzingatia misingi iliyoanishwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 katika utekelezaji wa Majukumu yao ya kila siku.
Bwana Kweka aliwasisitiza Madiwani hao ukjiepusha na vitendo vinavyopelekea uwepo wa mgongano wa Maslahi na kwamba wanatakiwa kuweka mbele masilahi ya Taifa badala ya kuweka mbele masilahi yao binafsi kitu ambacho ni kinyume na Maadili katika utendaji kazi wao wa kazi.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya Buchosa,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wengine wa Halmashauri hiyo.