JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
MAAFISA TEHAMA WATAKIWA KUWA MABALOZI KATIKA KUWAELEKEZA VIONGOZI MATUMIZI YA MFUMO WA ODS.
12 Feb, 2026
MAAFISA  TEHAMA   WATAKIWA  KUWA  MABALOZI  KATIKA KUWAELEKEZA VIONGOZI MATUMIZI YA MFUMO WA  ODS.

Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA  nchini wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika kuwaelekeza viongozi katika maeneo yao kuhusu matumizi ya mfumo wa ODS- (On Line Declaration System) ili kuwasaidia viongozi kujaza Matamko yao kwa njia ya mtandao kwa urahisi, umakini na kwa usahihi zaidi.

Kauli hiyo  imetolewa na  Katibu Msaidizi Kanda ya Kaskazini Arusha Bw. Gelard Mwaitebele  alipokuwa akifungua mafunzo ya Maadili kwa baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA kutoka katika mikoa ya  Arusha, Manyara na Kirimanjaro yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha tarehe 12 Februari 2026.

Bw. Mwaitebele katika hotuba yake amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wa pamoja na wa kina kuhusu matumizi ya mfumo wa ODS ili kuwasaidia viongozi walioko katika maeneo yao ya kazi kujaza Matamko yao kwa njia ya mtandao kwa weledi, usahihi na kwa umakini zaidi kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla,

Aidha, Bw. Mwaitebele katika hotuba yake amezitaja baadhi ya faida za matumizi ya mfumo huo kuwa ni pamoja na  kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa Umma kwa  kuwawezesha viongozi kuwasilisha Matamko yao kwa wakati na kwa haraka kwa kujaza mali zao pamoja na mali za wenza wao na mali za  watoto wao walio chini ya umri wa miaka 18 ambao awajaoa wala kuolewa.

Ametaja faida nyingine ya matumizi ya mfumo wa ODS  kuwa ni pamoja na kupunguza gharama na muda uliokuwa ukitumika katika ujazaji na uwasilishaji wa fomu kwa njia ya kawaida na kupunguza matumizi ya karatasi ngumu kama ilivyokuwa hapo awali pamoja na kuimarisha usalama na uhifadhi wa taarifa za viongozi kwa umakini mkubwa.

Bw. Mwaitebele ameongeza kuwa faida nyingine ya matumizi ya mfumo huu ni kurahisisha  ufuatiliaji na tathimini pamoja na kuharakisha  mchakato wa uhakiki na uchambuzi wa matamko na kuongeza ufanisi wa utendaji wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa ujumla wake.

“Ni muhimu kutambua kuwa, mafanikio ya mfumo huu yanategemea ushiriano wenu nyinyi wataalamu wa TEHAMA katika Taasisi zenu hivyo mnayo dhamana ya kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya teknolojia ipo sawa, changamoto za kiufundi zinatatuliwa kwa wakati na viongozi wanapatiwa mwongozo sahihi ambao mtaupata kupitia mafunzo haya”amesema.

Mafunzo haya yamewashirikisha  Wakuu wa vitengo vya TEHAMA kutoka katika Halmashauri, Jiji, Miji kutoka katika  mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Manyara.

Mafunzo haya yamewashirikisha  Wakuu wa vitengo vya TEHAMA kutoka katika Halmashauri, Jiji, Miji kutoka katika  mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Manyara.v

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >