JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Katibu Tawala Manyara Aagiza Shule zote kuwa na Klabu za Maadili
21 Apr, 2026
Katibu Tawala Manyara Aagiza Shule zote kuwa na Klabu za Maadili

 

Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Maryam Ahmed Muhaji amemuagiza Afisa elimu Mkoa wa Manyara kusimamia zoezi la kufungua Klabu za Maadili kila Shule na vyuo vilivyopo mkoani Manyara ili kuendeleza kukuza maadili mkoani humo.

Bi.Maryam ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Maadili kwa walimu walezi wa Klabu za Maadili mkoani Manyara yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara tarehe 21 Aprili, 2026.

“Pamoja na kuwa jukumu la malezi ya maadili yanaanzia nyumbani lakini ni wazi kuwa waalimu ndio mna mchango mkubwa katika kukuza maadili ya wanafunzi kwa sasa kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na tamaduni zetu, waalimu ndio mnabaki na watoto muda mrefu, hivyo Serikali inawategemea sana kwa hili.” alisema Bi. Maryam.

Aidha Bi. Maryam ameongeza kuwa mwanafunzi anapoingia shuleni uyo ni mtoto wa mwalimu, hivyo ni lazima tuanze kukumbushana maadili bora na lazima tuwafundishe namna jamii inavyoishi  kwani bila maadili ata ufaulu wa wanafunzi utashuka.

“Tumeshuhudia baadhi ya wanafunzi wanaaribikiwa shuleni wakati mzazi na mlezi wamejitahidi kumlea kwa weledi na hii ndio sababu inayopelekea sisi Serikali kupitia Sekretarieti ya Maadili kuanzisha Klabu za Maadili kwa kila shule,” alisema.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala huyo wa mkoa wa Manyara, jukumu la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni kusimamia na kukuza maadili tu, lakini wanaotengeneza maadili na kuweka msingi imara ni wazazi na walimu.

 

Aidha, Kiongozi huyo amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara kuhakikisha wanazilea klabu za maadili kwa kuhakikisha wanatenga bajeti ya kuziendeleza klabu hizi kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili.

Kwa upanda wake Mwalimu, Kassim Jamal kutoka Sekondari ya Qash katika Halmashauri ya wilaya ya Babati amesema utekelezaji wa agizo la Katibu Tawala wa Mkoa utakwenda kuwa chachu ya kuongeza ufaulu mkoani Manyara kwa kuwa maadili ndio msingi wa mambo mazuri.

Naye Katibu Msaidizi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini, Bw. Gerald Mwaitebele amempongeza Katibu Tawala wa Mkoa huo kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha maadili yanakuwa bora mkoani humo na amehaidi kuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma itashirikiana na Halmashauri zote za mkoani huo kuhakikisha shule  zinakuwa na Klabu za Maadili ambazo ni hai.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >