JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Kamishna wa Maadili awapika Viongozi wa Mkoa na Taasisi za Serikali Mkoani Mbeya kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma.
27 Oct, 2023
Kamishna wa Maadili awapika Viongozi wa Mkoa na Taasisi za Serikali Mkoani Mbeya kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kamishna wa Maadili awapika Viongozi wa Mkoa na Taasisi za Serikali Mkoani Mbeya kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Mbeya kwa kukutana na kuwasilisha mada kuhusu Maadili kwa viongozi wote wa Mkoa pamoja na Taasisi za serikali zilizopo mkoani humo.

Mkutano na viongozi hao ulifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wa Benjamin Mkapa na uliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Juma Homera.

Akiwasilisha mada kwa viongozi hao Mhe. Mwangesi alianza kwa kuitaja na kufafanua misingi ya Maadili ambayo ni pamoja na kuwa muadilifu; muwajibikaji; muwazi; muaminifu na mkweli; na kuheshimu Sheria.

Mhe. Mwangesi aliendelea kutaja misingi mingine ya maadili ambayo ni kuzingatia haki na usawa; kuzuia mgongano wa maslahi; kutunza siri; kufanya maamuzi kwa zingatia ubora na ufanisi.

Kwa mujibu wa Mhe. Mwangesi kiongozi au Mtumishi wa umma anategemewa kuwa na Maadili haya ya msingi ambayo yatasaidia uzingatiaji wa masharti ya sheria kuhusu Maadili ya viongozi wa umma na sheria nyingine za nchi.

“Misingi hii ya Maadili ndiyo inayojenga tabia na mienendo ya kimaadili inayopaswa kuzingatiwa na viongozi wote wanaoshika nafasi za madaraka zilizotajwa katika Sheria.Tabia na mienendo ya kimaadili ina mchango mkubwa katika kuepeusha uvunjaji wa Maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini” alifafanua Mhe. Kamishna.

Mhe. Mwangesi aliendelea kusema kuwa uzingatiaji wa viwango vya Maadili kwa viongozi wa umma unasaidia kuimarisha imani ya wananchi kuhusu uadilifu, haki na kutopendelea kwa Serikali.

Katika kuweka mkazo wa suala hili Mhe. Mwangesi alimnukuu Jaji L’Heureux – Dube wa Mahakama ya Juu ya Kanada kuwa kutokana na imani kubwa na wajibu unaoambatana na wadhifa wa ofisi ya umma, ni muhimu kwa maafisa wa serikali kuwajibika chini ya kanuni za Maadili ambazo kwa raia wa kawaida zingeonekana kuwa ni kali zaidi alisema Mhe. Mwangesi.

Katika mada yake Mhe. Mwangesi aligusia pia baadhi ya mambo yanayochochea ukiukwaji wa Maadili ambayo ni pamoja na tamaa; kukosa uaminifu; kukosa uzalendo; ubinafsi na Mgongano wa Maslahi; upokeaji wa zawadi zisizoruhusiwa na sheria na matumizi mabaya ya madaraka.

Akizungumza katika mkusanyiko huo wa viongozi wa Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera alisema kuwa Mkoa wa Mbeya kama zilivyo Taasisi nyingine za umma nchini unatekeleza Mkakati wa Udhibiti Rushwa Awamu ya Tatu wa mwaka 2017 hadi 2022.

Mhe. Homera aliendelea kusema kuwa utekelezaji wa Mkakati huo umelenga kukuza Uwajibikaji, Uwazi na Uadilifu katika matumizi ya rasilimali za umma kwa lengo la kuimarisha utoaji wa Huduma na ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa Mhe. Homera, kupitia mafunzo haya utawaongezea weledi kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Mbeya katika kutekeleza Mkakati wa kudhibiti Rushwa na Uadilifu katika Taasisi zote za umma zilizopo Mkoani Mbeya.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >