JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Jaji Mwangesi: Hauwezi kuwa Mwangalizi wa Maadili ya Wengine wakati wewe Mwenyewe hauna Maadili.
27 Oct, 2023
Jaji Mwangesi: Hauwezi kuwa Mwangalizi wa Maadili ya Wengine wakati wewe Mwenyewe hauna Maadili.

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wamekumbushwa kuzingatia maadili wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Wito huo umetolewa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa IACC jijini Arusha tarehe 14 Machi, 2021.

Mhe. Mwangesi alisema kuwa jukumu kubwa la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma, hivyo basi ni muhimu kwa watumishi wa Taasisi wakazingatia maadili na kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wengine wa umma katika Nyanja ya Uadilifu.

“Ninawaasa kwa mara nyingine kwa kuwa tumekubali kuwa watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma hatuna namna zaidi ya kuzingatia nidhamu, kuwa waaminifu na kupendana; atakayeenda tofauti na hayo atakuwa ameamua kuwa si miongoni mwetu na hatutasita kulichukulia hatua suala la namna hiyo”. Alisisitiza Mhe. Mwangesi.

Mhe. Mwangesi aliendelea kufafanua kuwa pamoja na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo katika kazi yao ya kusimamia uadilifu, aliwaomba watumishi hao wasikubali kuyumba au kuyumbishwa na hatimaye kutolewa kwenye mstari na badala yake waendelee kufuata misingi ya Weledi na Maadili katika utendaji kazi kwa kuepukana na rushwa na kushinda vishawishi vya rushwa na tamaa nyinginezo.

Akizungumzia lengo mahsusi la Mkutano huo alisema kuwa ni kupokea taarifa ya mapitio ya bajeti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Mwaka wa Fedha wa 2021/2022 na mwelekeo wa bajeti kwa mwaka 2022/2023.

“Ninatambua kuwa katika Taasisi yetu tuna mahitaji mengi na ya msingi na yote yanahitaji uwepo wa fedha.Kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali, ninaomba mipango na majadiliano yetu kuhusiana na bajeti ya mwaka 2022/2023 vizingatie vipaumbele vya Taasisi yetu pamoja na kazi zinazoonekana na kupimika”.Aliendelea kufafanua Mhe. Mwangesi.

Kwa upande mwinge, Mhe. Mwangesi alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuchukua tahadhali dhidi ya mlipuko wa homa ya mafua makali (UVIKO 19) kwa kuwaasa watumishi hao kuendelea kusikiliza na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa masuala ya afya kuhusiana na namna bora ya kujikinga dhidi ya mlipuko huo.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >