JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Fuateni Suluhu ya Vihatarishi kuepuka Madhara kwenye Taasisi.
30 Apr, 2025
Fuateni Suluhu ya Vihatarishi kuepuka Madhara kwenye Taasisi.

 

Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi amewataka watumishi kutafuta Suluhu ya vihatarishi vilivyopo katika Taasisi kuepuka madhara yanayoweza kuathiri taswira yake mbela jamii na Viongozi wa Umma.

Mhe. Mwangesi ametoa agizo hilo wakati akifungua kikao kazi cha kuhuisha daftari la viatarishi la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kilichowakutanisha wawakilishi kutoka kila Idara, Vitengo na Ofisi za Kanda mkoani Morogoro tarehe 30 Aprili, 2025.

Alisema, wakati mnafanyia kazi ya uhuishaji wa daftari, tunategemea utaisaidia Taasisi  kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya kisheria. Kikao kazi hiki kinapitia daftari la Viatarishi kutambua changamoto zinazokabili Taasisi katika utekelezaji wa majukumu na namna ya kupunguza uwezekano wa kutokea kwake.

“Ni imani yangu kuwa kazi hii ikifanyika vizuri tutafikia matarajio ya wananchi ya kuona viongozi waliopewa dhamana wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu ambalo ndilo lengo kuu la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Taifa kwa ujumla,” amesema.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Maadili, uhuishaji wa Dafrati la Vihatarishi, utasaidia Taasisi kuongeza tija kwa kutambua changamoto zinazoikabili na kuzitafutiai ufumbuzi.

“Zoezi hili liongeze tija ndani ya Taasisi, utendaji wetu wa kazi uendane na thamani ya fedha tunayotumia katika utekelezaji wa majukumu yetu,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Omary Juma amesema zoezi la uhuishaji wa daftari la Viatarishi utapunguza viatarishi vilivyopo ndani ya Taasisi na kuwa na kuongeza thamani ya fedha.

“Kazi hii inafanyika kwa kuangalia taswira ya Taasisi kwa ujumla na kutafuta ufumbuzi,” alisema.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Onesmo Mbekenga kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ametoa wito kwa Taasisi kuwa na mpango thabiti wa kupunguza viatarishi kwa kuweka katika mpango kazi wake wa kila mwaka.

 

 

 

 

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >