Je, Ofisi ya Maadili inawajibika vipi kwa wale Wabunge wanaotoa lugha chafu bungeni?
Je, Ofisi ya Maadili inawajibika vipi kwa wale Wabunge wanaotoa lugha chafu bungeni?
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.