Upokeaji wa Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni
Upokeaji wa Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni
13 Dec, 2023
08:00am-6:30pm
Ethics Secretariat Offices
ec@maadili.go.tz
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inapenda kuwakumbusha Viongozi wote wa umma walioainishwa kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Sura ya 398), kuwa zoezi la upokeaji wa Tamko la Rasilimali, Maslahi na Madeni kwa mwaka 2023, limeanza tangu tarehe 01 Oktoba, 2023 na litamalizika tarehe 31 Desemba, 2023.