Karibu kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Maadili.


Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni Taasisi ya Serikali inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais.Taasisi hii imeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 iliyotungwa na kuanza kutumika rasmi Julai,1995.